Friday, June 9, 2017




Details
by alanus
Created: Friday, 09 June 2017 08:56

SAFARI ya kusaka Nchi 15 zitazoungana na Wenyeji Cameroon kucheza Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika, AFCON 2019, inaanza Leo kwa Mechi za Kwanza za Makundi.
Yapo Makundi 12 ya Timu 4 kila moja na Mshindi wa kila Kundi atatinga moja kwa moja Fainali wakiungana na Washindi wa Pili wa Makundi Watatu Bora.


 

 Wenyeji Cameroon, ambao pia ndio Mabingwa Watetezi wa Afrika baada kutwaa AFCON 2017 huko Gabon, wamepangwa Kundi B lakini wao watakuwa wakicheza Mechi hizo kama ‘Kirafiki’ tu kwani wao kama Wenyeji hufuzu moja kwa moja kucheza Fainali.
Hivyo hata kama wao watwaa Ushindi wa Kundi B, Timu ya Pili ndio itahesabiwa kama Mshindi wa Kundi na kufuzu moja kwa moja.
Nchi yetu Tanzania ipo Kundi L pamoja na Cape Verde, Uganda na Lesotho.
Kesho Jumamosi Saa 2 Usiku, Tanzania, maarufu kama Taifa Stars, wako huko Azam Complex, Chamazi, kwenye Viunga vya Jiji la Dar es Salaam kucheza na Lesotho.
Mechi hii imehamishwa kutoka Viwanja vya Taifa na kile cha Uhuru vya Dar es Salaam Viwanja hivyo vyote Viwili vipo Matengenezoni.
++++++++++++++++++++++++++++
MAKUNDI:
A: Senegal, Equatorial Guinea, Sudan, Madagascar
B: Cameroon, Morocco, Malawi, Comoros
C: Mali, Gabon, Burundi, South Sudan
D: Algeria, Togo, Benin, The Gambia
E: Nigeria, South Africa, Libya, Seychelles
F: Ghana, Ethiopia, Sierra Leone, Kenya
G: DR Congo, Congo, Zimbabwe, Liberia
H: Ivory Coast, Guinea, Central African Republic, Rwanda
I: Burkina Faso, Angola, Botswana, Mauritania
J: Tunisia, Egypt, Niger, Swaziland
K: Zambia, Mozambique, Guinea-Bissau, Namibia
L: Cape Verde, Uganda, Tanzania, Lesotho
**Wenyeji wa Fainali za AFCON 2019, Cameroon, wapo Kundi B lakini wao wanafuzu moja kwa moja kucheza Fainali.
***Washindi wa kila Kundi na Timu za Pili zitakazomaliza Nafasi za Juu Bora 3 zitatinga Fainali
++++++++++++++++++++++++++++
Baada ya Mechi hizi za kwanza, Mechi za Pili za Makundi zitachezwa Machi 2018.
AFCON 2019
Ratiba
**Saa za Bongo
Ijumaa Juni 9      
22:00 Sudan v Madagascar [KUNDI A]
23:00 Libya v Seychelles [KUNDI E]
Jumamosi Juni 10     
15:30 Malawi v Comoros [KUNDI B]
16:00 Zambia v Mozambique [KUNDI K]
16:00 Burundi v South Sudan [KUNDI C]
16:30 Botswana v Mauritania [KUNDI I]
17:00 Cameroon v Morocco [KUNDI B]
18:00 Niger v Swaziland [KUNDI J]
19:00 Nigeria v South Africa [KUNDI E]
19:00 Guinea-Bissau v Namibia [KUNDI K]
19:30 Sierra Leone v Kenya [KUNDI F]
20:00 Tanzania v Lesotho [KUNDI L]
20:30 Congo, DR v Congo [KUNDI G]
20:30 Cape Verde v Uganda [KUNDI L]
21:00 Burkina Faso v Angola [KUNDI I]
22:00 Mali v Gabon [KUNDI C]
23:00 Ivory Coast v Guinea [KUNDI H]
23:00 Senegal v Equatorial Guinea [KUNDI A]
Jumapili Juni 11      
16:00 Zimbabwe v Liberia [KUNDI G]
17:00 Central African Republic v Rwanda [KUNDI H]
18:00 Benin v Gambia [KUNDI D]
18:30 Ghana v Ethiopia [KUNDI F]
Jumatatu Juni 12        
0:00   Algeria v Togo [KUNDI D]
1:00   Tunisia v Egypt [KUNDI J]

0 comments:

Post a Comment