Details
Created: Sunday, 25 June 2017 07:04
>LEO CHILE, GERMANY KUSONGA NUSU FAINALI?MABINGWA wa Ulaya Portugal Jana waliichapa New Zealand 4-0 huko Saint Petersburg Stadium, Mjini Saint Petersburg Nchini Russia, na kutinga Nusu Fainali ya Mashindano ya FIFA ya Kombe la Mabara.
Portugal ndio wametwaa ushindi wa Kundi A na sasa watacheza na Mshindi wa Pili wa Kundi B wakati Mexico, ambao Jana waliwapiga Wenyeji Russia 2-1 na kuwatupa nje, wakishika ushindi wa Pili wa Kundi B na sasa watacheza na Mshindi wa Kundi A kwenye Nusu Fainali.
Cristiano Ronaldo Jana alifungua Mabao ya Portugal kwa kufunga Penati katika Dakika ya 33 na Bao nyingine kupigwa na Mchezaji Mpya wa Man City Bernardo Silva, Andre Silva na Nani.
Mexico waliichapa Russia 2-1 kwa Bao za Dakika za 30 na 52 za Nestor Araujo na Hirving Lozano baada ya Russia kutangulia kwa Bao la Dakika ya 25 la Alexander Samedov.
++++++++++++++++
MSIMAMO:
++++++++++++++++
Leo zipo Mechi 2 za mwisho za Kundi B na Chile na Germany wote watatinga Nusu Fainali ikiwa hawatafungwa.
Kwenye Mechi hizo, Chile wataivaa Australia na Germany kucheza na Cameroon.
++++++++++++++++
FIFA KOMBE LA MABARA
Ratiba/Matokeo:
Hatua ya Kwanza
Jumamosi Juni 17
KUNDI A
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Russia 2 New Zealand 0
Jumapili Juni 18
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
Portugal 2 Mexico 2
KUNDI B
Spartak Stadium, Moscow
Cameroon 0 Chile 2
Jumatatu Juni 19
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
Australia 2 Germany 3
Jumatano Juni 21
KUNDI A
Spartak Stadium, Moscow
Russia 0 Portugal 1
Fisht Stadium, Sochi
Mexico 2 New Zealand 1
Alhamisi Juni 22
KUNDI B
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
Cameroon 1 Australia 1
Kazan Arena, Kazan
Germany 1 Chile 1
Jumamosi Juni 24
KUNDI A
Kazan Arena, Kazan
Mexico 2 Russia 1
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
New Zealand 0 Portugal 4
Jumapili Juni 25
KUNDI B
Fisht Stadium, Sochi
1800 Germany v Cameroon
Spartak Stadium, Moscow
1800 Chile v Australia
Hatua ya Pili
Nusu Fainali
Jumatano Juni 28
Kazan Arena, Kazan
2100 Portugal v Mshindi wa Pili Kundi B [NF1]
Alhamisi Juni 29
Fisht Stadium, Sochi
2100 Mshindi Kundi B v Mexico [NF2]
Mshindi wa 3
Jumapili Julai 2
Spartak Stadium, Moscow
1500 Atakaefungwa NF1 v Atakaefungwa NF2
FAINALI
Jumapili Julai 2
Saint Petersburg Stadium, Saint Petersburg
2100 Mshindi NF1 v Mshindi NF2
0 comments:
Post a Comment