
Serikali ya wilaya ya Ubungo imempa heshima Victor Wanyama ambae ni kiungo wa Tottenham na timu ya taifa ya Kenya kwa kuipa moja ya barabara za Ubongo jina la nyota huyo ambaye alikuwa mgeni wa heshima kwenye mchezo wa Ndondo Cup 2017 kati ya FC Kauzu dhidi ya Faru Jeuri.
Wanyama alipata fursa ya kwenda kuizindua barabara hiyo ambayo kwa sasa ipo kwenye matengezo ikifanyiwa ukarabati ili kuwa katika kiwango kizuri ukilinganisha na sasa.

Tumefarijika na jio wa Wanyama mchezaji kutoka timu ya Tottenham ya England na halmashauri ya Ubungo imempatia jina kwenye moja ya barabara zake ambazo zipo katika eneo hili kwa hiyo wanamichezo wote watakaokuwa wanakuja watakuwa wanaona jina la Victor Wanyama.” “Tunaamini barabara hii ambayo tumempa Wanyama itahamasisha wachezaji wengine kutoka mataifa mengine kuja Tanzania kwa kuwa tunawapokea vizuri.

Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Jacob Boniface amesema zawadi walioamua kumpa Wanyama itafanya wachezaji kutoka mataifa mengine kuja Tanzania kutokana na wageni wanavyopokelewa,
“Sisi tunashukuru na kama manispaa ya Ubungo tumepata hamasa kubwa ya michezo ambayo inafanyika kwenye maeneo ya Halmashauri ya manispaa ya Ubungo na kama unavyo jua ni halmashauri mpya na watu wanavyofurika namna hii kupitia michezo nafarijika sana.”

0 comments:
Post a Comment