Emanuel Okwi amesaini mkataba wa miaka miwili (2) kujiunga na Simba kuanzia msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara pamoja na mashindano mengine ikiwa ni pamoja na michuano ya Afrika (Caf Confederatio Cup).
Okwi aliwasili Dar Juni 24, 2017 usiku akiwa ameambatana na mke wake na kupokelewa na Makamu wa Rais wa Simba Geoffrey Nyange Kaburu.
Inaelezwa kwamba, baada ya kusaini mkataba na Simba, Okwi atarejea tena Uganda kisha atakuja Tanzania kikazi kwa ajili ya maandalizi ya msimu ujao 2017-2018.
Hii imekua ni taarifa njema kwa mashabiki wengi wa Simba ambao wanaamini uwepo wa Okwi kwenye kikosi chao kutaongeza nguvu na mafanikio zaidi kwenye msimu ujao.
0 comments:
Post a Comment