Saa chache baada ya aliyekuwa golikipa wa
Azam FC Aishi Manula kutangazwa kuondoka katika club hiyo na kujiunga na club ya
Simba,
Azam FC usiku wa leo wametangaza mbadala wake.
Azam FC leo wamemtangaza golikipa
Benedict Haule aliyekuwa akiichezea
Mbao FC ya
Mwanza kuwa mbadala wa
Aishi Manula aliyejiunga na
Simba,
Benedict amesaini mkataba wa miaka miwili.

Benedict Haule akisaini mkataba mbele ya Meneja Mkuu wa Azam FC Abdul Mohammed na Meneja wa timu Philip Alando.
Hii sio mara ya kwanza kwa
Benedict Haule kuichezea
Azam FC alikuwa akiichezea timu ya vijana ya
Azam FC ambapo alikulia katika Academy ya timu hiyo, hivyo kurejea kwake ni sawa na kusema ameamua kurudi nyumbani.
0 comments:
Post a Comment