Mchezaji wa tenisi anayeorodheshwa
nambari miongoni mwa wanawake Serena Williams amepiga picha za utupu
katika kurasa ya kwanza ya jarida la August Vanity Fair.
Nyota
huyo wa tenisi alibaini kwamba alikuwa akitarajia mwanawe wa kwanza na
mpenziwe Alexis Ohanian kabla ya michezo ya Australia Open mnamo mwezi
Januari.Aliambia jarida hilo kwamba hakutarajia chochote hadi alipobaini kwamba alikuwa mgonjwa wakati wa mazoezi.
Serena alifanya vipimo hivyo wakati alipokuwa akipigwa picha na kampuni moja ndani ya Hoteli moja nchini Australia na kusema kuwa alipigwa na butwaa wakati alipopata majibu.


Rafikiye Jessica baadaye alitumwa kununua vifaa vyengine vitano vya kupima uja uzito ili kumthibitishia Serena kwamba ni mjamzito.
Vipimo vyote vilithibitisha.Habari hiyo pia ilisema vile Serena na mpenziwe walivyokutana 2015.

Alimchumbia Disemba katika meza hiyo hiyo ya Cavalieri katika hoteli moja huko Italy ambapo walikutana.
0 comments:
Post a Comment