Details by alanus
Created: Tuesday, 13 June 2017 06:49
HIVI sasa yupo Vakesheni, lakini James Rodriguez, Jina la
Utani James Bond, anatafakari nini hatima yake huku akimaliza Msimu bila kunena
lolote kwa wenzake wa Real Madrid n ahata Bodi ya Klabu.
Hadi sasa, si Mchezaji mwenyewe,
wala Wakala wake Jorge Mendes, aliefunguka nini kitajiri licha kuwepo na
minong’ono mingi kuhama kwake kutoka Real.
Hata Kocha Zinedine Zidane amefunga
Ofisi nae kwenda Vakesheni hajatamka lololote kuhusu Rodriguez mbali ya kutaka
Kikosi chake kilichotwaa Ubingwa La Liga na Ulaya kubaki vile vile.
Hata hivyo, Klabu ya Real imeliweka
Dau la anaemtaka Rodriguez kuwa wazi na nalo ni EURO Milioni 75.
Dau hilo limekausha nia ya Klabu
nyingi Ulaya kuingia mbioni kumsakaingawa duru za ndani ya Real Madrid
zimedokeza kuwa ni Mabingwa wa England pekee, Chelsea, ndio wameonyesha nia ya
kumnunua
0 comments:
Post a Comment