Wakuu wa chama cha
soka cha Saudi Arabia wameomba msamaha baada ya timu ya taifa hilo
kutoshiriki katika kukaa kimya dakika moja kwa heshima waathiriwa wa
shambulio la London Bridge.
Wachezaji wa Australia walishikanisha
mikono yao kama ishara ya heshima kabla mechi hiyo ya siku ya Alhamisi
ya kufuzu kwa Kombe la Dunia iliyochezewa katika uwanja wa Adelaide Oval
uliopo kaskazini mwa Australia.Wachezaji wa Saudi walionekana kujishughulisha zaidi na kujipangia nafasi uwanjani.
Mbunge mmoja wa Australia ametaja kisa hicho kama ''cha aibu''.
Viongozi wa soka wamesema walikuwa wamearifiwa hapo awali kwamba mila na ''tamaduni za Australia hazikuwa zinaambatana na mila za Wasaudia.''
Chama cha soka cha Saudi Arabia kiliomba radhi siku ya Ijumaa.
''Wachezaji hao hawakuwa na madhumini ya kutoheshimu makumbusho ya waathiriwa ama kusababisha ghadhabu kwa familia zao, marafiki au mtu yeyote aliyeathirika na mkasa huo,'' walisema katika taarifa.
''Chama cha soka cha Saudi Arabia kinalaani vitendo vyote vya kigaidi na kutoa salamu zao za rambirambi kwa familia za waathiriwa, serikali na watu wote wa Uingereza.''
oka la Australia (FFA), waliosema walikuwa wamearifiwa
hapo awali kwamba wachezaji wa Saudia ''wangeheshimu mila zetu wakiwa
uwanjani.''Wanasiasa kadhaa wa Australia waliishtumu timu ya Saudia.
''Huu ni ukosefu wa heshima na nilifikiri ni jambo la aibu.''
Raia wawili wa Australia , Kirsty Boden na Sara Zelenak walikuwa miongoni mwa watu wanane waliofariki katika mashambulio hayo.

0 comments:
Post a Comment