Juzi usiku kocha Arsene Wenger aliwaambia mashabiki wa klabu hiyo kwamba Sanchez na Mustafi wako njiani na siku ya Jumapili watarejea London kuanza mazoezi.
Habari hiyo iliwafurahisha sana mashabiki wa Arsenal kwani wengi hawakuamini kama Sanchez anaweza kurejea tena katika timu yao na kufanya nao mazoezi.
Wakati zikiwa zimebaki siku mbili tu ili Sanchez arejee, amepata homa ya ghafla. Kupitia ukurasa wake wa Instagram Sanchez amepost picha na kuandika “sick”.
Habari hii ni mbaya kwa mashabiki wa Arsenal kwani wameanza kukata tamaa kuhusu kurudi kwa Sanchez kwa maana hawezi kurudi Jumapili tena kama ilivyosemwa na itabidi wasubirie apone.
Mkataba wa Arsenal na Sanchez umebakiza mwaka mmoja tu na inadaiwa Alexis hataki kuendelea kucheza Arsenal lakini kocha wake naye hataki aondoke katika dirisha hili.
0 comments:
Post a Comment