- Details by alanus
- Created: Tuesday, 11 July 2017 13:00
DOMINIC SOLANKE: LIVERPOOL YAMSAINI KINDA WA CHELSEA
Liverpool wamekamilisha kumsajili Straika Tineja wa Chelsea Dominic Solanke baada ya Mkataba wake na Chelsea kumalizika na Kinda huyo kugomea Mkataba Mpya.
Hata hivyo, Chelsea wanapaswa kulipwa Ada kwa vile walimkuza Kijana huyo wa Miaka 19 na Jopo Maalum litaamua kiasi cha kulipwa na kinakisiwa kuwa Pauni Milioni 3.
Mapema Mwezi huu, Solanke alifunga Bao 5 wakati Timu ya Taifa ya England U-20 ikitwaa Kombe la Dunia la U-20 huko South Korea.
Msimu wa 2015/16, Solanke alikuwa kwa Mkopo huko Belgium kwenye Klabu ya Vitesse Arnhem na kupachika Bao 7 katika Mechi 25.
Akiwa na Chelsea, Solanke aliichezea Mechi 1 tu akitokea Benchi kwenye UEFA CHAMPIONZ LIGI dhidi ya NK Maribor Oktoba 2014.
EVERTON WAJITAYARISHA KUMNUNUA CHRISTIAN BENTEKE
Baada ya kumuuza Romelu Lukaku kwa Manchester United, Everton sasa wako mbioni kumnunua Straika wa Crystal Palace Christian Benteke ili ajumuike na Wachezaji wao wengine Wapya Sandro Ramirez na Wayne Rooney.
Benteke, ambae pia anafuatiliwa na Chelsea, aliihamaLiverpool na kwenda Palace Msimu uliopita ambako aliifungia Bao 17.
ROMELU LUKAKU YUPO TAYARI 'KUTOBOA UKUTA' KWA AJILI YA JOSE MOURINHO
Mchezaji Mpya wa Manchester United Romelu Lukaku ametamba kuwa yupo tayari ‘kutoboa Ukuta’ kwa ajili ya Jose Mourinho.
Jana Lukaku alijumuika kwa mara ya kwanza na Kikosi cha Man United ambacho kipo Mazoezini huko UCLA Jijini Los Angeles, USA.
Hii itakuwa ni mara ya pili kwa Lukaku na Mourinho kufanya kazi pamoja baada ya kuwa wote huko Chelsea.
Alipoulizwa kama Mourinho alichangia kwa yeye kuhamia Man United, Lukaku alijibu: Yeah, alichangia. Tuna uhusiano mzuri na nipo tayari kupenya Ukutani kwa ajili
0 comments:
Post a Comment