SHIRIKISHO
la Ngumi za Kulipwa Duniani (WBC) limemaliza utata kwa kusema kwamba
majaji walikuwa sahihi kumpa ushindi bondia Jeff Horn wa Australia dhidi
ya Manny Pacquiao wiki iliyopita mjini.
Horn
alimpokonya bondia wa Ufilipino taji la WBC uzito wa Welter baada ya
ushindi wa majaji wote watatu kwa pointi 117-111, 115-113 na 115-113,
lakini wengi wakasema bondia wa umri wa miaka 29 'alibebwa' kwa sababu
alikuwa anapigana kwenye ardhi ya nyumbani.
WBO ikakubali kupitia upya matokeo na leo imetoa matokeo, ambayo yanaendelea kumtambua Horn kama mshindi.
WBO imemaliza utata kwa kusema Jeff Horn ni mshindi halali wa pointi dhidi ya Manny Pacquiao PICHA ZAIDI GONGA HAPA
"Matokeo ya pambano la Jeff Horn na Manny Pacquiao yalikuwa na utata, yakasababisha kuwagawa mashabiki. Kwa sababu hii, uwazi ni muhimu mno," imesema WBO katika taarifa yake.
"Kwa hili, majaji watano ambao hawakutajwa, majaji wa kiwango cha juu kutoka nchi tofauti walitakiwa kuangalia tena pambano bila sauti. Kujua mshindi wa kila raundi, majaji watatu kati ya watano wanapaswa kukubaliana.
"Kutokana na matokeo, inaweza kufahamika kwamba Pacquiao alishinda raundi tano, wakati Horn alishinda raundi saba,".
Wakati
kumekuwa na mazungumzo kwamba mkongwe wa umri wa miaka 38, Pacquiao
anaweza kustaafu, pambano la marudiano liliandikwa katika mkataba na
wawili hao wanatarajiwa kurudiana baadaye mwaka huu.
Mwalimu
wa zamani wa shule, Horn, ambaye sasa rekodi yake imekuwa kushinda
mapambano 17 na kupigwa moja baada ya kumpiga bingwa wa dunia wa
madaraja nane ya uzito tofauti amefarijika na taarifa ya WBC.
"Inanipa
ushahidi nyuma yangu kwamba naweza kutumia sasa"alisema akizungumza na
Waandishi wa Habari Uwanja wa Ndege wa Brisbane leo na kusema sasa
anaamini alishinda pambano hilo kihalali.
0 comments:
Post a Comment