Jimbo la Los Angeles limeteuliwa
rasmi kuandaa mashindano ya Olimpiki ya wakati wa majira ya joto mwaka
2028 katika makubaliano yatakayoihakikishia Paris kuandaa Olympiki ya
mwaka 2024.
Miji yote miwili ilikuwa akipigania kuwa mwenyeji wa mashindano hayo makubwa duniani katika tarehe za awali.Rais wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki Thomas Bach amesema anakaribisha uamuzi huo wa Los Angeles kukubali kuwa mwenyeji wa mashindano hayo kwa tarehe za mbele.
Kamati hiyo ya Olimpiki imesema itatoa mchango wake wenye thamani ya dola bilioni 0.8 kwa mji wa Los Angeles ili kufidia gharama zitakazoongezeka.
0 comments:
Post a Comment