WAZIRI Mkuu wa Uholanzi, Mark
Rutte, ametangaza kuwa, michezo
yote ndani ya nchi hiyo imesimamishwa hadi Septemba Mosi, mwaka huu.
Kutokana na hilo,
inamaanisha kwamba Ligi Kuu ya Uholanzi maarufu Eredivisie pamoja na ligi
zingine nazo zimepigwa ‘teke’ hadi muda huo, hivyo hakutakuwa na michezo kwa
takribani miezi mitano ijayo.
Viwanja vyote vya soka
vitatakiwa kufunguliwa Septemba Mosi, hivyo msimu huu wa 2019/20 nao utaendelea
muda huo. Kwa sasa hapana. Hii yote inatokana na uwepo wa janga la corona.
"Ni ngumu, lakini
tunapaswa kufanya hivyo," alisema Rutte.
Hadi ligi hiyo inasimamishwa, timu
nyingi zilikuwa zimecheza mechi 26 na kubakiwa na nane tu kumaliza msimu huu wa
2019/20 huku vinara wakiwa Ajax waliocheza mechi 25 na kukusanya pointi 54 sawa
na AZ Alkmaar wanaoshika nafasi ya pili.
0 comments:
Post a Comment