BEKI
wa kati wa timu ya Ruvu Shooting ya mkoani Pwani Santos Mazengo amesema
kuwa, kwa sasa yupo huru kufanya mazungumzo na timu yoyote kwa kuwa
mkataba wake na timu hiyo unaisha mwishoni mwa msimu huu.
Mazengo ameongeza kuwa, anaikaribisha timu yoyote inayohitaji huduma
yake kufanya nayo mazungumzo kwa ajili ya msimu ujao wa ligi
Mazengo aliyesajiliwa na Ruvu Shooting misimu miwili iliyopita akitokea
kikosi cha vijana cha timu hiyo amekuwa katika kiwango kikubwa msimu
huu na ameweza kuisadia timu yake kwa kiwango kikubwa.
Aidha mchezaji huyo amesema kuwa anaipa nafasi ya kwanza timu yake ya
Ruvu Shooting kufanya mazungumzo naye kama watataka kuendelea kupata
huduma yake.
“Kwa sasa nipo huru kufanya mazungumzo na timu yoyote kwani mkataba
wangu unaisha mwishoni mwa msimu huu, hivyo nazikaribisha timu zozote
zinazohitahiji saini yangu”,alisema Mazengo
0 comments:
Post a Comment