Thursday, April 23, 2020


BEKI Muitalia, Marco Materazzi, amemchana vibaya kocha wake wa zamani, Rafael Benitez.
Wawili hao walikutana kwenye kikosi cha Inter, ikiwa ni baada ya mwaka 2010 timu hiyo kuchukua ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya chini ya Kocha Jose Mourinho.
"Ndani ya Inter, siyo kwamba Benitez utawala wake ulianza vibaya na kumalizika vibaya, bali haukuisha kabisa.
"Alitibua kila kitu ambacho Mou [Jose Mourinho] alikijenga.
"Alipofika alijaribu kuwaweka kando wale wote ambao walionekana kuwa na sauti katika chumba cha kubadilishia nguo, hapo ndipo shida ilipoanzia," alisema Materazzi.
Materazzi akishangilia na Mourinho.
Beki huyo wa zamani wa Everton, alimsifia Mourinho kwa kumtolea mifano Benitez kwamba alishinda kutatua matatizo.
"Kipindi cha Mourinho wote tulikuwa na ushirikiano.
"Alifanya mambo makubwa yenye faida. Kama mtu anapenda kuondoa yale ya zamani na kuleta mambo mapya kwa ajili ya faida ya klabu, namuheshimu, lakini Benitez alijaribu tu kuondoa kila kitu cha Jose, hiyo ilitusumbua.
"Mtu ambaye ameshinda ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Ulaya akiwa na Liverpool mbele ya Milan lazima atakuwa na uelewa wa hali ya juu, lakini ndani ya Inter, Benitez alikuwa na matatizo makubwa na mimi, alipoenda Napoli akasumbuana na Paolo Cannavaro, kule Chelsea ugomvi ukawa na John Terry, Real Madrid alikorofishana na Cristiano Ronaldo.
"Je! Hapo ni makosa ya wengine kila wakati? Kwa hivyo, nilimshukuru kila wakati kwa sababu nilijaribu kuchukua fursa ya makosa hayo na kujifunza," alimaliza Materazzi.

0 comments:

Post a Comment