- Details
- Created: Tuesday, 18 July 2017 12:25

Wilshere amebakiza Mwaka Mmoja kwenye Mkataba wake na Arsenal na Msimu ulopita alikuwa kwa Mkopo huko Bournemouth.
Hata hivyo Mchezaji huyo mwenye Miaka 25 na ambae ameichezea
England mara 34 hakumaliza Msimu baada ya kuvunjika Mguu kwenye Mechi na
Tottenham Mwezi Aprili.
Pia iliwahi kuripotiwa kuwa Wilshere atapelekwa kwa Mkopo huko Crystal Palace.
Lakini Wikiendi iliyopita Meneja wa Arsenal Arsene Wenger alieleza
kuwa anatarajia Wilshere atabaki Arsenal na kupigania namba yake.
0 comments:
Post a Comment