
Mshambuliaji wa Arsenal Alexis
Sanchez hajamwambia mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger kwamba anataka
kuondoka katika klabu hiyo , kulingana na mkufunzi huyo ambaye
anatarajia mchezaji huyo wa Chile kukamilisha kandarasi yake.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 28 amesalia na mwaka mmoja katika kandarasi yake na Arsenal.Hatahivyo imeripotiwa kwamba Sanchez angependa kujiunga na wapinzani wa Arsenal Manchester City .
Alipoulizwa iwapo Sanchez alimwambia kwamba angependelea kuondoka , rais huyo wa Ufaransa amesema kuwa hapana.
Wenger aliongezea: Wachezaji wana kandarasi na tunawatarajia kuheshimu kandarasi zao , hilo ndio tunalotaka.
Sanchez alijiunga na Arsenal kutoka Barcelona kwa kitita cha pauni milioni 35, 2014.
0 comments:
Post a Comment