
Mshambuliaji wa Brazil Neymar
amesema kuwa alihitaji changamoto mpya , wakati anapojiunga na klabu ya
PSG kutoka Barcelona kwa kitita kilichovunja rekodi ya uhamisho cha
(£200m).
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25 alishinda mataji
saba muhimu katika misimu yake minne katika uwanja wa Nou Camp ikiwemo
taji la klabu bingwa mara moja na lile la La Liga mara mbili.Amesema kuwa babake Neymar Sr alimtaka kusalia Barcelona.
''Nimeshinda mataji yote niliohitajika kushinda'' ,alisema Neymar ambaye atapokea mshahara wa (£40.7m) kwa mwaka katika kipindi cha miaka mitano.
Akiandika katika mtandao wake wa Instagram, aliongezea: Nimeshinda mataji yote ambayo mchezaji soka anafaa kupata.
- Kwa nini Neymar anataka kuondoka Barcelona?
- Neymar awapiku Messi, Ronaldo na Pogba kwa thamani
- Je unaweza kununua nini kwa thamani ya Neymar ?
''Na kwa mara ya pili katika maisha yangu, nitaenda kinyume na matakwa ya babangu''.
Uhamisho wa Neymar umevunja rekodi ya awali iliowekwa na Paul Pogba aliporudi kuichezea Manchester United kutoka Juventus kwa kitita cha £89m mnamo mwezi Agosti 2016.
Mshahara wake wa £782,000- kwa wiki unamaanishi kuwa PSG itamlipa £400m.
Neymar anatarajiwa kuzinduliwa mbele ya mashabiki wa PSG katika uwanja wa Parc des Princes siku ya Jumamosi.
0 comments:
Post a Comment