Aliyekuwa bingwa wa dunia katika
ndondi Wladmir Klitschko amestaafu katika ndondi na hivyobasi kufutilia
mbali uwezekano wowote wa mechi ya marudiano dhidi ya Anthony Joshua.
Raia
huyo wa Ukraine mwenye umri wa miaka 41 alipigwa knockout katika raundi
ya 11 na bingwa wa sasa Joshua katika uwanja wa Wembley mnamo mwezi
Aprili .Joshua mwenye umri wa miaka 27 alitumai kwamba Klitschko atashiriki mechi ya marudiano mjini Las Vegas tarehe 11 mwezi Novemba.
Klitschko ambaye ni bingwa mara mbili wa uzani mzito duniani
anakamilisha mapigano yake akiwa ameshinda mara 64 na kushindwa mara 5.
0 comments:
Post a Comment