Image caption
Raisi wa kamati ya Olimpiki Thomas Bach aliyeko
katikati akitangaza wenyeji wa michuano hiyo kwa mwaka 2024 na 2028
akiwa na meya wa mji wa Paris Anne Hidalgo aliyeko kushoto na meya wa
mji wa Los Angeles Eric Garcetti aliyeko kulia
Kamati ya Olimpiki
ya Kimataifa imechagua mji mkuu wa ufaransa, Paris, kuwa mwenyeji wa
michuano ya Olimpiki mwaka 2024, na kuutunuku mji wa Los Angeles nchini
Marekani kuwa mwenyeji wa michuano hiyo mwaka 2028 .
Mwezi uliopita, kamati hiyo ilifanya maamuzi ya kuwa
Olimpiki mbili za majira ya joto zitatolewa kwa wakati mmoja, baada ya
miji kadhaa kuahirisha zabuni zao kutokana na wasiwasi wao kuhusu
ukubwa, gharama, na utata wa kuandaa moja ya matukio makubwa kama hayo
ya michezo duniani. Rais Emmanuel Macron wa Ufaransa amesema kuwa
uchaguzi wa mji wa Paris kuwa mwenyeji wa michuano hiyo ni ishara kwamba
ya kutambuliwa kwa mji na nchi kitu ambacho kila Mfaransa anapaswa
kusherehekea.
0 comments:
Post a Comment