Sunday, October 8, 2017


Sibusizo Vilakazi wa Afrika Kusini akisherehekea bao lake dhidi ya Burkina FassoHaki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionSibusizo Vilakazi wa Afrika Kusini akisherehekea bao lake dhidi ya Burkina Fasso
Afrika Kusini ilijipatia matokeo mazuri katika kampeni yake ya kutaka kufuzu katika kombe la dunia baada ya kuifunga Burkina Faso 3-1 mjini Johannesburg.
Percy Tasu aliwapatia wenyeji uongozi wa mapema , Themba Zwane akaongeza idadi hiyo na kuwa mabao mawili baada ya nusu saa kabla ya Sibusizo Vilakazi kufanya mambo kuwa 3-0 kabla ya kipindi cha kupumzika.
Bongani Zungu alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja katika dakika ya 69 kwa ukosefu wa nidhamu kufuatia mgogoro.
Mchezaji wa Burkina Faso Alain Traore alikuwa na bahati kusalia uwanjani baada ya kumpiga kisukusuku Zungu.
Mchuano kati ya Uganda na Ghana ambao ulikwisha 0-0Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
Image captionMchuano kati ya Uganda na Ghana ambao ulikwisha 0-0
Kwengineko wenyeji Uganda na Black Stars ya Ghana walilazimika kutoka sare ya 0-0 katika mechi ya kufuzu kwa dimba la dunia la 2018 katika uwanja wa Nelson Mandela mjini Nambole , matokeo ambayo yanapunguza matumaini yao ya kufuzu kwa dimba hilo la Urusi.

0 comments:

Post a Comment