Bingwa wa zamani wa uzito wa juu Tyson Fury amesema hatoomba tena leseni ya kupigana kutoka chama cha ndondi nchini Uingereza BBBC.
Furry mwenye miaka 29 alinyang'anywa leseni yake Oktoba 2016 baada ya kugundulika kutumia dawa zilizokataliwa michezoni.
Aliandika katika ukurasa wake wa Twitter kwamba hata kama alikutwa na kosa lakini hawezi kunyenyekea kupata haki yake.
''Kwa namna walivyochukulia mambo haya, hapana sitaendelea kuomba, asante.'' Alisema Furry.
Uamuzi wake wa kutoomba tena leseni hiyo kunaweka njia panda mustakabali wake katika mchezo huo, licha ya awali kusema ana mpango wa kuachana nao
0 comments:
Post a Comment