Thursday, October 5, 2017


Halep anasema hakutarajia kumshinda Sharapova ndani ya muda mfupi hivyo
Image captionHalep anasema hakutarajia kumshinda Sharapova ndani ya muda mfupi hivyo
Mchezaji namba mbili katika tenis nchini Romania Simona Halep ameweka historia yake kwa mara ya kwanza kwa kumsinda Maria Sharapova katika michuano ya China Open hatua ya robo fainali.
Halep alihitaji dakika 73 kumsinda Sharapova kwa seti 6-2 6-2.
Katika mchezo huo, Sharapova alishindwa kabisa kufurukuta na mwisho wa mchezo akasema Halep alikuwa mzuri kushinda yeye.
Halep kwa sasa atakutana na Daria Kasatkina wa Urusi ambaye alimchapa Agnieszka Radwanska kwa seti 4-6 7-5 6-2.
Mara ya mwisho kwa Sharapova kumshinda Halep ilikuwa katika michuano ya US Open mwezi Agosti.

0 comments:

Post a Comment