Tuesday, October 3, 2017

Arsene Wenger akizungumzia kuhusu barcelona kujiunga na ligi ya Uingereza

Image captionArsene Wenger akizungumzia kuhusu barcelona kujiunga na ligi ya Uingereza
Baada ya kikosi chake kupata ushindi wa 2-0 dhidi ya Brighton and Hove Albion, mkufunzi wa Arsenal Arsene Wenger alitoa maoni yake kuhusu uwezekano wa Barcelona kujiunga na ligi ya Premier , akikiri kwamba itafanya mambo kuwa magumu zaidi.
Kutokana na hali ya kisiasa huko Catalonia, kulikuwa na uvumi kuhusu kule ambako Barcelona itacheza iwapo italazimika kuondoka la Liga.
Wenger aliulizwa kuhusu uwezekano huo wa kucheza nchini Uingereza na ni nini angefanya iwapo hilo lingefanyika.
''Ningejifunza kuelewa Kicatalan'', aliwaambia wanahabari.
''Iwapo Barcelona inataka kujiunga na ligi ya Uingereza itafanya mambo kuwa magumu zaidi kwa kila mtu''.
''Lakini sidhani kwamba wamefikia uamuzi huo, ni swala la kuvutia na kuwa na visa kama hivyo kwa upande wa michezo kwa kuwa Barcelona ni klabu ya kisiasa''.
Mabingwa wa la Liga Barcelona
Image captionMabingwa wa la Liga Barcelona
Na alipoulizwa iwapo angeikaribisha katika ligi ya Uingereza, raia huyo wa Ufaransa alisema ingekuwa muhimu iwapo wangeangazia klabu nyengine za nyumbani iwapo wangetaka kupanua ligi hiyo.
''Nadhani ingevutia kuona vile itakavyokuwa katika ligi ya championship'',aliongezea.
''Tuna vilabu vya kutosha takriban 20 lakini iwapo unataka kuongeza vilabu hivyo hadi 24 ni vyema kuvialika vilabu vya Uskochi kabla ya kuelekea Uhispania''

0 comments:

Post a Comment