
Mwendeshaji baiskeli wa Rwanda Areruya Joseph ameshinda mashindano ya Tour of Rwanda.
Areruya
Joseph, 21, anayechezea timu ya Dimension Data ya Afrika Kusini
ameibuka mshindi wa mashindano ya kimataifa ya mbio za baiskeli maarufu
Tour Of Rwanda yaliyomalizika jana mjini Kigali.Mashindano hayo yalikuwa ya kuzunguka sehemu 7 tofauti za nchi hiyo, umbali wa kilomita 821.
Arerura Joseph amemshinda mpinzani wake wa karibu Mueritrea Eyob Metkel akimzidi kwa sekunde 28.

Mashindano haya yalishirikisha waendeshaji baiskeli 73 kutoka timu 16 za mataifa mbali mbali duniani lakini wakamaliza waendesha baiskeli 43.
0 comments:
Post a Comment