Manchester City
ilionyesha mchezo mwengine mzuri katika ushindi dhidi ya Leicester ambao
umeimarisha uongozi wake katika kilele cha jedwali la ligi ya
Uingereza.
Kikosi cha Pep Guradiola kiliendeleza msururu wake wa
matokeo mazuri baada ya likizo ya mechi za kimataifa kwa kujipatia
ushindi wa 16 mfululizo katika mashindano yote kupitia uongozi wa
mshambuliaji wao Gabriel Jesus kabla ya kiungo wa kati De Bryuine
kufunga mkwaju mkali ambao kipa wa Leicester alishindwa kuuona.Wakati huohuo mabingwa watetezi Chelsea walipata ushindi rahisi dhidi ya West Brom na kumuongezea presha kocha wa West Brom Tony Pulis.
Alvaro Morata alifunga bao lake la nane katika ligi baada ya kufunga mpira uliopanguliwa na kipa Ben Foster kufuatia shambulio la Eden Harzard.

Katika kipindi cha pili Harzard alifunga bao lake la pili kutoka maguu 18 baada ya kupata pasi nzuri kutoka kwa fabregas.
Kwengineko Mohamed Salah aliendeleza umahiri wake kwa kuipatia Liverpool mabao mawili huku timu hiyo ikiilaza Southampton kwa urahisi na kujipatia ushindi wa tatu mfululizo kwa mara ya kwanza 2017.

Mshambuliaji huyo aliipatia timu hiyo ya nyumbani bao la pili kufuatia pasi ya Phillipe Coutinho.
Hakuna mchezaji wa ligi ya Uingereza mwenye mabao mengi katika mashindano yote kama Salah msimu huu na ijapokuwa alitulia baada ya kipindi cha kwanza Coutinho alichukua uongozi na kufunga kufuatia mpira uliopanguliwa na kipa baada ya shambulizi la Roberto Firmino.

0 comments:
Post a Comment