“Nilihisi kama nilikuwa nacheza dhidi ya ulimwengu mzima wa soka.”

Haya ndio maneno ya Edgardo Andrada, golikipa wa kiargentina alivyokuwa akielezea mchezo ambao Pele alikuwa analisaka goli la 1,000 katika ardhi ya nyumbani kwao Brazil. Ilikuwa saa 11:11 jioni mnamo tarehe 19 November 1969, wakati akijiandaa kucheza penati ya Pele. Siku hii hakuwa akiichezea timu yake ya Taifa vs Selecao au timu ya kutoka nje ya Brazil.
Edgardo Andrada alikuwa kipenzi cha mashabiki wengi waliojaza kwenye uwanja wa Maracana. Timu yake ya Vasco Da Gama walikuwa wanatoa sare ya 1-1 nyumbani dhidi ya Santos, huku zikiwa zimebaki dakika 12 kabla ya mchezo kumalizika.
“Kelele zilikuwa kubwa sana, zingeweza kukupa ukiziwi, cha kushangaza hata mashabiki wengine wa Vasco Da Gama walikuwa dhidi yangu mimi kipa wao.”
Unajiuliza kwanini? Jibu ni kwamba mfalme wa soka, alikuwa akipiga penati ambayo angefunga ingekuwa anatimiza magoli 1,000 rasmi.

Pele alikuwa na magoli 999 kabla ya mchezo huo. Matokeo ya mchezo yalikuwa hayana umuhimu kama tukio la Pele la kihistoria. Umati wa mashabiki 65,000 ulijitokeza uwanjani ukitegemea kuona Pele akitengeneza historia ya kuwa mchezaji wa kwanza kutimiza magoli 1,000.
“Asilimia kubwa ya mashabiki waliojaza Maracana walitaka kuwa sehemu ya historia kwa kushuhudia goli hilo, wachezaji wa Vasco Da Gama walifanya kila njia kuhakikisha hilo halitokei siku hiyo,” Pele anakumbuka.
“Walikuwa wanazuia vikali dhidi yangu, walinichezea sana rafu, huku wakiwa wananiambia sitofunga siku hiyo. Lakini ilikuwa imepangwa kutokea siku hiyo. Ilibidi litokee jambo fulani ili niweze kupata nafasi ya kufunga na likatokea.”

Pele akachukua mpira na kuelekea kwenye
eneo la kupigia penati, akajaribu kupiga mpira kuelekea upande aa kulia
pembeni kabisa, Andrada akajirusha na kufanikiwa kuhusa mpir lakini
ukamzidi nguvu na kutinga nyavuni.
“Kwa
mara ya kwanza katika maisha yangu ya kucheza soka, nilikuwa na
wasiwasi mkubwa. Andrada alikuwa kwenye kiwango kikubwa. Sikuwahi kuwa
na presha kama siku hiyo. Nilikuwa natetemeka. Lakini nikafanikiwa
kupiga mpira na ukatinga nyavuni……. uwanja ukalipuka kwa kelele za
mashabiki.”

Pele akakimbilia ndani ya nyavu wa na kuubeba mpira, namba kubwa ya waandishi wa habari wakaingia uwanjani kwenda kupiga picha.
Baadhi ya mashabiki wakaingia nao
uwanjani na kwenda kumpa Pele jezi ya Vasco Da Gama ikiwa imeandikwa
namba 1000. O Rei (The King) akaivaa na kukimbia uwanjani pembeni kuwapa
salamu ya heshima mashabiki huku akifuatiliwa na mamia ya mashabiki.
Golikipa Andrada pia alitokwa na machozi mfululizo baada ya tukio hilo. “Nilihuzunishwa sana,” anasema golikipa huyo ambaye baadae alienda kumkumbatia Pele na kumpongeza.
“Nilikuwa nataka sana kuiokoa ile penati. Sikutaka kuwa golikipa ambaye
historia ingemkumbuka kwamba ndio aliyefungwa goli la 1000 na Pele.”

Baada ya tukio hili la kihistoria,
ilimchukua refa dakika zipatazo 25 ili hali itulie na kuendelea na
mchezo. Dakika zilipomalizika, Santos wakafanikiwa kushindwa 2-1. Hakuna
aliyejali matokeo hayo. 19 November 1969 was ilikuwa siku yenye tukio moja tu kubwa katika historia ya ufungaji magoli katika soka.
0 comments:
Post a Comment