Hali ya kiungo mnyumbulikaji wa Arsenal Santiago Carzola inasikitisha sana, tumekuwa tukitaraji habari nzuri kutoka kwa madaktari wanaomtibu Carzola lakini taarifa iliyotoka inaumiza sana.
Ni mwaka na zaidi sasa kiungo huyo yuko nje ya uwanja na jambo linalosikitisha zaidi ni kwamba ameshafanyiwa oparesheni nanw ili kutibu tatizo lake la mguu na mwezi ujao alipaswa kuanza mazoezi.
Lakini kupitia mtandao wake wa Twitter Carzola ametoa ujumbe ambao umewaumiza watu wengi, Carzola anasema bado anasikia maumivu katika mguu wake na hii inamfanya arudi tena hospitali kwa oparesheni ya tisa.
Matatizo
yanayomkumba Carzola yanaonekana madogo kwa kuyazungumzia lakini watu
wake wa karibu ikiwemo Arsene Wenger anasema ni majeruhi mabaya kuwahi
kuyaona tangu aanze kufundisha soka.
Nahodha
wa timu ya taifa Hispania Sergio Ramos amemtumia ujumbe Carzola wa
kumtia nguvu katika kipindi hiki kigumu anachopitia na kusema kwamba
dunia bado inahitaji kuona akitoa burudani ndani ya uwanja.

0 comments:
Post a Comment