Kocha Arsene Wenger atatumikia adhab ya kukosa mechi tatu England
KOCHA wa Arsenal, Arsene Wenger amefungiwa
mechi tatu na kupigwa faini ya Pauni 40,000 kwa kumtolea maneno makali
refa kwenye chumba cha kubadilishia nguo baada ya mchezo dhidi ya West Bromwich Jumapili iliyopita.Wenger
alikasirika baada ya refa Mike Dean kuwazawadia The Baggies penalti ya
dakika ya mwisho baada ya mpira uliopigwa na Kieran Gibbs kumfikia
mkononi Calum Chambers.
Alimfuata
Dean baada ya mechi na kuanza kumtolea maneno ya kulaumu uamuzi wake
baada ya Jay Rodriguez kufunga penalti hiyo kuipatia timu yake sare ya
1-1.
Wenger
alifunguliwa mashitaka na Chama cha Soka England mapema wiki hii na
sasa atakosekana kwenye mechi ya Raundi ya Tatu Kombe la dhidi ya
Nottingham Forest Jumapili na mechi ya kwanza ya Nusu Fainali ya Kombe
la Ligi, maarufu kama Carabao dhidi ya Chelsea.
0 comments:
Post a Comment