Leo Februari 26, 2018 mshambuliaji wa Simba Emanuel Okwi ameivunja rekodi ya Simon Msuva na Abdulrahman Musa baada ya kufikisha magoli 16 kwenye ligi kuu Tanzania bara ikiwa ni mzunguko wa 19 raundi ya pili msimu huu (2017/18).

Msuva na Abdulrahman walifunga magoli 14 kila mmoja na kuibuka wafungaji bora msimu uliopita.

Okwi aliifikia rekodi yao kwenye mchezo ambao Simba ilikuwa ugenini kucheza na Mwadui mechi ambayo ilimalizika kwa sare ya 2-2. Katika mchezo wa leo ambao Simba imeshinda 5-0 dhidi ya Mbao, Okwi amefunga magoli mawili ambayo yamemfanya aivunje rekodi hiyo.

Hadi sasa Okwi bado anaendelea kuongoza kwenye orodha ya wafungaji wa msimu huu akiwa na magoli 16 akifuatiwa na Obrey Chirwa mwenye magoli 11 huku John Bocco akiwa na magoli 10 katika nafasi ya tatu.

Magoli ya Simba yamefungwa na Shiza Kichuya dakika ya 38, Emanuel Okwi akafunga goli la pili kwa mkwaju wa penati dakika ya 41 kisha akafunga tena dakika 70, Erasto Nyoni akafunga goli la nne dakika 82 na goli la tano likafungwa na Nicholas Gyan.

Mechi ya tano Mbao imekutana dhidi ya Simba, Mbao haijawahi kupata ushindi bata mara moja. Imepoteza mechi nne na kupata sare moja.

- Oktoba 20, 2016 Simba 1-0 Mbao
- Aprili 10, 2017 Mbao 2-3 Simba
- Mei 27, 2017 (fainali-ASFC) Simba 2-1 Mbao
- Septemba 21, 2017 Mbao 2-2 Simba
- Februari 26, 2018 Simba 5-0 Mbao
0 comments:
Post a Comment