KIUNGO wa Manchester United, Ander Herrera anakabiliwa na mashitaka ya kiungo cha miaka minne jela nchini Hispania kwa tuhuma za kupanga matokeo katika La Liga.
Waendesha
mashitaka wa Hispania wamesema walitaka kifungo cha miaka miwili jela
na kufungiwa kucheza soka kwa miaka sita kwa kiungo huyo na wachezaji
wengine 35 katika kesi iliyofunguliwa tena Mahakama ya Valencia mapema
mwezi huu.
Kifungo cha miaka miwili jela kwa mara ya kwanza kwa Hispania huwa mtu hawekwi gerezani, maana yake ikiwa Herrera atashitakiwa kwa makosa ya rushwa mchezoni ataepuka jela.
Kiungo wa Manchester United, Ander Herrera yuko hatarini kwenda jela miaka minne kwa tuhuma za kupanga matokeo La Liga PICHA ZAIDI GONGA HAPA
Lakini
Jumatatu, ikabainika kwamba wanasheria wa Ligi hiyo kubwa Hispania,
ambao pia wamechukua hatua dhidi ya wachezaji waliohusishwa kwenye
uchunguzi wa Mei mwaka 2011 kutokana na mechi baina ya timu ya zamani wa
Herrera, Zaragoza na Levante, walitaka adhabu kubwa zaidi ya
wanasheria wa Serikali kama watakutwa na hatia ya rushwa.
Magazeti
yenye heshima yakiwemo la kila siku, Las Provincias yamesema kifungo
cha miaka minne jela — kifungo cha kawaida kinachowezekana — ni sehemu
ya mashitaka waliyofungua wanasheria wa La Liga katika Mahakama ya
Maelekezo Namba Nane ya Valencia.
Deportivo
La Coruna, timu iliyoteremka Daraja kutokana na ushindi wa Zaragoza wa
2-1 ugenini dhidi ya Levante bado haijawasilisha mashitaka yake na
vyanzo vilisema kwamba hawakuwa tayari kusema watafanya hivyo lini.
Gazeti
la Las Provincias limesema kwamba wanasheria wa La Liga pia wanataka
faini kwa wachezaji ya Pauni Milioni 2.56 kwa kila mmoja, zaidi ya
Milioni 1.7 zinazotakiwa na waendesha mashitaka wa Serikali kama
watuhumiwa watakutwa na hatia.
Wachezaji
wengine wanaokabiliwa na tuhuma hizo mbali ya Herrera ni pamoja na
nyota wa Atletico Madrid, Gabi, mshambuliaji wa zamani wa
Middlesborough, Cristhian Stuani na Javi Venta, ambaye alimalizia soka
yake Brentford.
Kocha wa wakati huo wa Zaragoza, Javier Aguirre na mmiliki wa zamani, Agapito Iglesias wote wanachunguzwa.
Tume
ya Rushwa ya Hispania imesema katika kurasa zake 17 kwamba fedha
walizolipwa wachezaji tisa wa Zaragoza akiwemo Herrera na klabu hiyo
zilirejeshwa taslimu na zinaweza kuwa walikabidhiwa wachezaji wa
Levante.
Waendesha
mashitaka wa Serikali wamesema walikubali kupoteza mechi hiyo ya Mei
21, mwaka 2011 na kuwasaidia wapinzani wao waepuke kushuka Daraja
watakapopokea malipo ya Pauni 852,000.
Herrera
alisema mapema mwezi huu kwamba; "Kama nilivyosema mwaka 2014 suala
hili lilipoibuka, sijafanya na sitafanya, chochote kupanga matokeo ya
mchezo.
"Ikiwa
nitaitwa kujieleza popote, nitafurahi kuhudhuria kwa sababu dhamira
yangu ni nzuri kabisa. Naipenda soka na ninaamini juu ya mchezo wa
kiungwana - kote, ndani na nje ya Uwanja,".
Watuhumiwa wengine wote nao wamekata kufanya uchafu wowote.
0 comments:
Post a Comment