Wednesday, February 28, 2018

Kombe la Dunia


Wakenya wamejitokeza kwa wingi kulitazama na kupigwa picha na Kombe la Dunia la Shirikisho la Soka Duniani (Fifa) ambalo limekuwa nchini humo kwa siku mbili.
Kombe la Dunia
Raia waliruhusiwa kulitazama kombe hilo likiwa ndani ya sanduku la kioo katika ikulu, Nairobi siku ya Jumatano.
Wengi walitumia simu zao kupiga picha, kujiwekea kumbukumbu.
Kombe la DuniaRais wa Kenya Uhuru Kenyatta alilipokea rasmi kombe hilo la dhahabu katika ikulu ya Nairobi Jumanne.
Ni rais huyo pekee aliyeruhusiwa kuligusa pekee nchini Kenya. Kando na marais, ni wachezaji waliowahi kushinda kombe hilo pekee ambao huruhusiwa kuligusa.
Haki miliki ya picha PSCU
Haki miliki ya picha AFP/Getty
Kombe hilo linatembezwa mataifa mbalimbali kabla ya michuano ya Kombe la Dunia kuanza Juni nchini Urusi.
Ni mara ya tatu kwa kombe hilo kuwa Kenya, awali ikiwa 2010 na 2013 katika ya fainali zilizofanyika Afrika Kusini na Brazil.
Mwaka 2010, lilipokelewa na rais wa wakati huo Mwai Kibaki ambaye alistaafu mwaka 2013.
Kenya ni ya 21 mwaka huu kuwa mwenyeji wa kombe hilo mwaka huu kati ya mataifa 51 yanayotarajiwa kulipokea kabla ya Juni.
Kombe la DuniaKombe hilo ambalo lina uzani wa kilo 6.1 limeelekea Maputo, Msumbiji.
Wakati wa kuwasili kwa kombe hilo Jumanne, wacheza ngoma waliovalia mavazi ya kitamaduni ya jamii ya Wamaasai walikuwepo kuwatumbuiza wageni.
Uhuru Kenyatta
Baadhi walitumia fursa hiyo kupiga picha zao kwa kutumia simu.
Kenyatta
Picha/AFP, Getty na PSCU

0 comments:

Post a Comment