Ajenti wa kiungo wa kati wa Man United Paul Pogba amewasilisha ombi la kuhama la mchezaji huyo katika klabu kubwa za Ulaya .
Mchezaji
huyo wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 24 alianza mechi ya United ya 0-0
dhidi ya Sevilla siku ya Jumatano akicheza kama mchezaji wa ziada.
(Sports Illustrated)
Courtois amekiri kwamba ajenti wake atasikiliza ombi kutoka timu hiyo ya La Liga.. (Mirror)

Manchester United ina hamu ya kumsajili kiungo wa kati wa Dinamo Zagreb mwenye umri wa miaka 19 Nikola Moro, ambaye ametajwa kuwa 'Luka Modric mpya' (Talksport)

Mshambuliaji wa Real Madrid Karim Benzema, 30, ananyatiwa na klabu nne za Ufaransa ikiwemo Lyon, Paris St-Germain lakini mchezaji huyo hapendelei kuondoka. (AS)

West Bromwich Albion inamchunguza meneja wa klabu ya Ostersunds Graham Potter. Raia huyo wa Uingereza mwenye umri wa miaka 42 anasema kuwa anapanga kufunza katika ligi ya Uingereza katika siku za usoni. (Daily Mail)

Mchezaji wa zamani wa Newcastle na Tottenham David Ginola amepata mtoto mwengine akiwa na umri wa miaka 51 miaka miwili baada ya kupata mshutuko wa moyo wakati wa mechi ya hisani. (BirminghamLive)
0 comments:
Post a Comment