Kamati ya Maadili ya TFF iliyokutana Februari 3, 2018 na
Februari 17, 2018, katika ofisi za TFF Karume, pamoja na mambo mengine
yaliyojadiliwa pia ilipitia na kutoa hukumu ya tuhuma za kutoa taarifa
zisizo sahihi na kughushi leseni za usajili zilizowakabili watuhumiwa
mbalimbali walioletwa mbele yake.
Tuhuma hizo zilitokana na mechi namba 26 Kundi A ligi daraja la
kwanza iliyofanyika Oktoba 29, 2017 kati ya Mvuvumwa FC na Friends
Rangers ambapo katika mchezo huo timu ya Mvuvumwa FC iliwachezesha
wachezaji watano (5) ambao ni Elias Costa Elias (jezi namba 5), Lukwesa
Joseph Kanakamfumu (jezi namba 7), Dunia Abdallah Dunia (jezi namba 1),
Doto Justine Kana (jezi namba 12) na Mwarami Abdala Mwarami (jezi namba
8).
Kamati imemtia hatiani kocha na mratibu wa Mvuvumwa FC Joseph
Kanakamfumu kwa makosa yote mawili, kutoa taarifa zisizo sahihi,
(udanganyifu) ili kufanikisha usajili wa wachezaji kinyume na taratibu
za ligi daraja la kwanza.
Kosa la kwanza Kanakamfumu akiwa kocha wa Mvuvumwa FC aliwaorodhesha
wachezaji (Elias Costa Elias, Lukwesa Joseph Kanakamfumu, Dunia Abdallah
Dunia, Doto Justine Kana Mwarami Abdala Mwaram) kushiriki mechi namba
26 huku akijua kwamba hawana leseni halali kutoka TFF, wachezaji wote
walitoka katika kituo ‘academy’ anayoiendesha hivyo ni dhahiri alijua
alichokuwa anakifanya.
Kosa la pili Kanakamfumu aliamua kuwaongeza wachezaji hao baada ya
kukabidhiwa timu kwa vile alifahamu uwezo wao na inaonekana alitumia
uzoefu wake katika mpira wa miguu kupata leseni za kughushi.
Kwa makosa hayo, kamati inamfungia Joseph Kanakamfumu kutojihusisha na shughuli za mpira wa miguu kwa kipindi cha miaka mitano.
Home
»
»Unlabelled
» TFF imemfungia kocha miaka 5 kujihusisha na soka
Wednesday, February 28, 2018
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
0 comments:
Post a Comment