Imekuwa ni wiki yenye furaha kwa Mreno, Cristiano Ronaldo baada ya kuvuta mkwanja mrefu kutoka klabu ya Juventus wakati mashabiki wa vibibi hao wa Turin wakimiminika kununua jezi za staa huyo.

Rasmi Cristiano Ronaldo ajiunga na Juventus ya Italia
Jezi halisi ya Ronaldo ambayo imetengenezwa na klabu ya Juventus ambazo ni za mechi za nyumbani zinagharimu kiasi cha dola 144.95 ambayo ni sawa na Tsh 329715.16.

Jezi hiyo hiyo ya nyumbani ya Ronaldo kopi yake ambayo siyo origino inauzwa kwa kiasi cha dola 104.95 sawa na Tsh 238687.62

Wakati kwa watoto jezi hiyo ya nyumani unaweza kuinunua kwa dola 79.95 ambayo ni sawa na Tsh 181,848.64.

Wakati mshahara wa mwalimu hapa nchini kima cha chini ni sawa na Tsh 331000 kwa mwezi.
Ronaldo mwenye umri wa miaka 33, ameingia kandarasi ya pauni milioni 105 kutua Juventus siku ya Jumanne akitokea Real Madrid.

Ronaldo
alikutana na rais wa timu ya Juventus, Andrea Agnelli mchana wa siku ya
Jumanne kwenye hoteli huko Greece ambapo alikuwa mapumzikoni na mpenzi
wake pamoja na familia kabla ya kukubali dili hilo la miaka minne ambalo
atavuna kiasi cha pauni 500,000 kwa wiki.

Hapo
jana siku ya Alhamisi nyota huyo ameonekana akifurahia maisha na
familia yake akiwa sambamba na marafiki zake akiposti picha kwenye
instagram inayo muonyesha akipata chakula cha usiku.

0 comments:
Post a Comment