Maurizio
Sarri ametangazwa rasmi kuwa meneja mpya wa klabu ya Chelsea na kurithi
mikoba ya Antonio Conte ndani ya Stamford Bridge.

Conte
ametimuliwa hapo jana siku ya Ijumaa baada ya ufalme wake wa miaka
miwili kwenye klabu hiyo iliyopo Magharibi mwa jiji la London.

Sarri
ameachana na timu yake ya zamani ya Napoli na kutua Chelsea baada ya
kuinoa kwa misimu mitatu klabu hiyo inayo shiriki ligi ya Serie A huku
aliyekuwa meneja wa Chelsea Carlo Ancelotti akitarajiwa kupokea kijiti
cha kukinoa kikosi hicho.

Mara
baada ya utambulisho huo Sarri amesema kuwa anajisikia mwenye furaha
kuwa ndani ya Klabu ya Chelsea na ninafasi nyingine katika taaluma yake
ya ufundishaji.

Sarri
anatarajia kusafiri siku ya Jumatatu hadi nchini Australia kwaajili ya
kukutana na kikosi cha wachezaji wa Chelsea pamoja kujiunga na benchi
zima la ufundi akiwemo mchezaji wa zamani wa timu hiyo Gianfranco Zola.
0 comments:
Post a Comment