Staa wa soka wa timu ya taifa ya
Ureno Cristiano Ronaldo jioni ya July 15 2018 amewasili mjini
Turin Italia kwa ajili ya kukamilisha usajili wake wa kujiunga na club ya
Juventus ya
Italia, hiyo ikiwa ni siku chache zimepita toka
Juventus wafikie makubaliano na
Real Madrid.

Ronaldo, Mama yake mzazi, mtoto wake wa kwanza Ronaldo JR na mpenzi wake Gio kwa nyuma wakiwasili Turin.
Ronaldo amewasili
Turin kwa ajili ya kukamilisha usajili wake ambapo atasaini
Juventus mkataba wa miaka minne na Jumatatu ya July 16 2018 atatambulishwa rasmi kama mchezaji wa
Juventus kwa dau la usajili la euro milioni 100 huku
Real Madrid wakikubaliana na
Juventus kuongezewa euro milioni 12 katika kipindi cha miaka miwili.

Ronaldo akiwa na mpenzi wake Gio
0 comments:
Post a Comment