
Real Madrid inajiandaa kutoa dau la £60m kumnunua mlinda lango wa Tottenham na Ufaransa Hugo Lloris, 31. (Sun)
Bilionea
wa Urusi Alisher Usmanov anataka kuuza asilimia 30 ya hisa zake katika
klabu ya Arsenal baada ya kukiri kwamba mmiliki mkuu wa klabu hiyo Stan
Kroenke hatomwachia udhibiti wa klabu hiyo. (Financial Times)
Manchester United na Chelsea zimewasilisha ombi la kutaka kumsaini kiungo wa kati wa Bayern Munich na Uhispania Thiago Alcantara, 27, ambaye anapatikana kwa dau la £62m. (ESPN)
Tottenham na Chelsea huenda zikamnyatia winga wa Ufaransa Anthony Martial, 22, ambaye anataka kuondoka katika klabu ya Manchester United lakini kusalia katika ligi ya Premia. (Sun)
Chelsea huenda ikamkosa mshambuliaji wa Juventus Gonzalo Higuain, 30, huku wapinzani wao wa Serie A AC Milan wakiwa na hamu ya kumsajili raia huyo wa Argentina kwa dau la £57m. (Evening Standard)
Fulham imekubali makubaliano ya kumsaini mchezaji wa Ujerumani na winga wa zamani wa Chelsea Andre Schurrle, 27, kutoka Borussia Dortmund. (West London Sport)
Liverpool itamzuia mshambuliaji Daniel Sturridge, 28, msimu huu na iko tayari kumpoteza mchezaji huyo wa Uingereza msimu ujao kwa uhamisho wa bure (Liverpool Echo)
Wolves wanatarajiwa kumsaini winga wa Uhispania Jonny Castro, 24, kwa mkopo wa muda mrefu kutoka knblau ya Atletico Madrid. (Mail)
Derby imeanza mazungumzo ya kutaka kumsaini mshambuliaji wa Uingereza mwenye umri wa miaka 28 Martyn Waghorn kutoka klabu mwenza ya ligi ya mabingwa Ipswich kwa dau la £8m. (Mail)
Fenerbahce wamewasilisha ombi la kumsaini mshambuliaji wa Tottenham na Uholanzi Vincent Janssen, 24, ambaye alihudumu msimu uliopita kwa mkopo katika klabu hiyo ya Uturuki . (SkySports)
Mkufunzi wa zamani wa Uingereza Sven-Goran Eriksson, 70,ameanza mazungumzo ya kuchukua ukufunzi wa timu ya taifa la Iraq. (Sky Sports)
Tetesi za soka Ulaya Jumanne 24.07.2018
Mshambuliaji wa
zamani wa Arsenal Thierry Henry, ambaye yuko katika kikosi cha ukufunzi
cha Ubelgiji amekubali kwa maneno kuchukua uoingozi wa klaby ya Aston
Villa akichukua mahala pake Steve Bruce. (Daily Star)
Chelsea
inajiandaa kuimarisha dau la £45m kumnunua beki wa Juventus na Itali
Daniele Rugani, 23, baada ya ombi la hapo awali la £36m kukataliwa.
(Goal)
Arsenal bado ina hamu ya kumsajili kiungo wakati wa Sevill aliyeshinda kombe la dunia Steven Nzonzi, 29,lakini hawako tayari kuafikia matakwa ya kandarasi ya raia huyo wa Ufaransa ya kumuachilia kwa dau la £35m. (France Football)

Tottenham ina matumaini ya kujipatia £30m kupitia kumpiga bei mshambuliaji wa Uholanzi Vincent Janssen, 24, pamoja na mshambuliaji wa Uhispania Fernando Llorente, 33. (Evening Standard)
Newcastle iko katika mazungumzo kumsajili beki wa Deportivo La Coruna na Uswizi Fabian Schar, 26, ambaye ana kandarasi inayomzuia yenye thamani ya £3.5m . (Daily Mail)
Klabu mpya iliopanda katika ligi ya Premia Fullham imewasilisha ombi la kutaka kumnunua mshambuliaji wa Brazil na Real Sociedad Willian Jose, 26 kwa dau la £26m. (Sun)
West Ham na Leicester zote zinamnyatia kiungo wa kati wa Juventus na Itali ,25, Stefano Sturaro. (La Gazzetta dello Sport - in Italian)
Barcelona, Juventus na idadi kubwa ya klabu za Premia zinamtaka winga mwenye umri wa miaka 20 Ismaila Sarr. Rennes inataka kulipwa £50m ili kumpiga bei mchezaji huyo wa Senegal (Sun)
West Brom wanakaribia kumnunua kiungo wa kati wa Uingereza Harvey Barnes, 20, kwa mkopo kutoka Leicester. (Leicester Mercury)
0 comments:
Post a Comment