Kauli
ya Akilimali imekuja tena kutokana na uongozi wa Simba jana kutangaza
kuwa itafanya uchaguzi wake Novemba 3 2018 ili kupata viongozi wapya
ambao watachukua nafasi za waliomaliza muda wao.
Mzee
huyo ameongea kwa jazba akishangaa kuwa mpaka sasa Yanga haijafanya
uchaguzi wakati ndiyo ilikuwa klabu ya kwanza kupaswa kufanya hivyo.
Katibu
huyo ameeleza kushangazwa na namna Yanga wanachokitaka huku akisema ni
jambo la kushangaza kwa maana hata klabu ya Coastal Union tangu iamuliwe
na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kufanua uchaguzi ilikamilisha
haraka.
Aidha,
Akilimali amesema mpaka sasa aliyekuwa Mwenyekiti wao, Yusuf Manji,
hajasema kama amerejea na kwa mujibu wake haoni haja ya kumbembeleza mtu
ambaye hana nia ya kurejea.
Yanga
na Simba zote zilipewa siku 75 za kuanza mchakato wa uchaguzi na TFF na
Simba wametangaza jana tarehe rasmi ya uchaguzi huo ambapo fomu
zitaanza kutolewa leo kunako makao makuu ya klabu hiyo yaliyopo
Msimbazi, Dar es Salaam.
0 comments:
Post a Comment