JOSE Mourinho kwa sasa anafikiria kurejea kwenye benchi la ufundi akiwa ni meneja endapo atapata timu sahihi.
Mourinho
mwenye miaka 56 amekuwa bila timu kwa muda mrefu baada ya kupigwa chini
ndani ya kikosi cha Manchester United, Desemba mwaka jana.
Amekuwa
akihusishwa kujiunga na timu ya Benfica msimu ujao, Lyon na Newcastle
United wametajwa kumhitaji bosi huyo ambaye ameinoa pia Chelsea na Real
Madrid.
"Mpango
wangu kurejea kazini upo na nina hasira ya kazi ila kwa sasa ninasubiri
timu sahihi ambayo nitaifundisha nikiwa na mipango sahihi.
"Wakati
sahihi ukifika nitafanya mambo ambayo nimewahi kuyafanya ninapenda kazi
na ninapenda pia michezo mingine mbali na mpira naona kwa sasa ni muda
wangu wa kufurahia," amesema.
0 comments:
Post a Comment