BRENDAN Rodgers bosi wa Leicester City amethibitisha kwamba tayari timu yake imeachana na ofa za timu mbili ambazo zilikuwa zinahitaji huduma ya beki wao wa kati Harry Maguire.
Licha
ya ofa hizo mbili kwa nyota huyo wa Taifa la England ambaye alikuwa
sehemu ya kikosi kilichocheza mchezo wa kirafiki dhidi ya Scunthorpe
siku ya Jumanne na waliibuka na ushindi wa bao 1-0.
Maguire
amezivutia timu nyingi kubwa ikiwa ni pamoja na Manchester United na
Manchester City ambao walikuwa wanahitaji huduma yake kwa dau la thamani
ya pauni milioni 90.
"Harry
ni mchezaji wa thamani ya juu na ana uwezo mkubwa inakuwa ni ngumu kwa
sasa timu kukubali kumuuza, zipo timu ambazo zinamhitaji ila bado
tunaona ni kijana mzuri kwetu na ana uhakika wa kupata namba kama
ambavyo alifanya kwenye dakika 45 alizocheza," amesema.
0 comments:
Post a Comment