Mshambuliaji wa Manchester United Marcus Rashford, leo ameibuka mchezaji
bora wa mchezo wa kirafiki dhidi ya Leeds ambao ni maalumu kwa ajili ya
maandalizi ya msimu ujao.
United kwa sasa wameweka kambi nchini Australia na kwenye mchezo wa leo wameibuka na ushindi wa mabao 4-0.
Kocha Mkuu, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa ameshangazwa na uwezo wa
Rashford ambaye ametupia pia bao pamoja na kinda Mason Greenwood ambaye
ametupia bao lake la kwanza, mabao mengine yalifungwa na Phil Jones
pamoja na Martial.
Mchezaji aliyechaguliwa na mashabiki kuwa mchezaji bora kwa mchezo wa leo ni kiungo mshambuliaji Paul Pogba.
0 comments:
Post a Comment