Manchester United
imeafikiana na Leicester makubaliano ya thamani ya £80m kumsajili Harry
Maguire na kumfanya kuwa mlinzi mwenye thamani kubwa katika historia.
United
italipa £60m kumsajili mchezaji huyo mwenye miaka 26 - atakayefanyiwa
ukaguzi wa kiafya leo Jumatatu - na £20m za ziada katika siku zijazo.
(Sun)Leicester inatarajiwa kuijaza nafasi ya Maguire kwa kumsajili mchezaji wa Brighton Lewis Dunk, baada ya kuafikiana kwa mkataba wa thamani ya £45m kwa mchezaji huyo wa miaka 27. (Sun)
Celtic imekataa ombi la Arsenal la hivi karibuni linalokisiwa kuwa na thamani ya £25m - ili kumsajili beki wa kushoto mwenye miaka 22 Kieran Tierney. (Sky Sports)
- Fainali Afcon 2019: Ni Senegal dhidi ya Algeria
- Pogba agoma kuongea na waandishi
- Cheza: Nani mshindi AFCON kwa mambo mengine kando na soka?
Tottenham na Arsenal zimejiunga na Manchester City katika kumfukuzia beki kamili wa Brazil Dani Alves mwenye umri wa miaka 36, ambaye ni ajenti huru tangu alipoondoka Paris St-Germain. (Mundo Deportivo kupitia Daily Mail)

Mchezaji anayelengwa na Arsenal, Everton mwenye umri wa miaka 23 anayeichezea Gremio, anasema amepewa pendekezo lakini amekataa kufichua jina la klabu iliyomfuata. (Mirror)
Meneja wa Liverpool Jurgen Klopp anasema klabu hiyo itaendelea kuweka wazi matumaini yake kuhusu kumsajili beki wa kushoto kuichukua nafasi ya mchezaji wa kimataifa wa Uskotchi Andrew Robertson, mwenye umri wa miaka 25, wakati wa dirisha la uhamisho msimu wa joto. (ESPN)

Mchezaji wa kiungo cha kati wa Liverpool Herbie Kane, anatarajiwa kukamilisha uhamisho wa mkopo kwenda katika klabu ya ubingwa wiki hii. Brentford, Charlton na Hull zote zinataka kumsajili mchezaji huyo wa miaka 20 aliyeichezea Doncaster msimu ulioipita. (Goal)
Bora za Jumapili 14.07.2019:

Barcelona wamemuhakikishia wakala wa Coutinho kuwa hawana mpango wa kumuuza mchezaji huyo, japo anadai kuwa mteja wake anawekwa sokoni na wawakilishi walio karibu kabisa na klabu hiyo. (Sky Sports)
Liverpool pia wamejiunga kwenye mbio za kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Fedor Chalov mwenye thamani ya pauni milioni 20. Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na Manchester United pia wanamnyemelea mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Mirror)
Mchezaji ghali zaidi duniani wa Paris St-Germain, Neymar, amekoleza uvumi kuwa anarudi Barcelona baada ya kuachia video anayoonekana amevaa jezi ya Barca, pamoja na mistari ya biblia yenye mafumbo. (Goal.com)

Beki wa Leicester na England Harry Maguire, 26 - ambaye anahusishwa na uhamisho kwenda Man United kwa dau la £75m - ameambia klabu yake kuwa anataka kuondoka. (Mail)

Kiungo mchezeshaji wa Tottenham na timu ya taifa ya Denmark Christian Eriksen, 27, yawezekana akaendelea kusalia kwenye klabu hiyo ya jijini London baada ya kuwa na uhaba wa klabu ambazo zimeonesha nia ya kumsajili. (Guardian)

Kiungo wa Everton na Senegal Idrissa Gueye, 29, amesema anafahamu juu ya tetesi zinazomhusisha na uhamisho kwenda PSG lakini kwa sasa amedai malengo yake yapo AFCON. (Sport Witness)
Arsenal wapo Tayari kuminyana na Tottenham na Juventus katika mbi za kumsajili kiungo waklabu ya Roma ya Italia Nicolo Zaniolo, 20. (Calciomercato)
Liverpool pia wamejiunga kwenye mbio za kinyang'anyiro cha kutaka kumsajili mshambuliaji wa CSKA Moscow Fedor Chalov mwenye thamani ya pauni milioni 20. Arsenal, Manchester City, Tottenham, Chelsea na Manchester United pia wanamnyemelea mchezaji huyo mwenye miaka 21. (Mirror)
0 comments:
Post a Comment