Saturday, September 21, 2019

Mchezaji wa zamani wa Real Madrid Angel di Maria alifunga magoli mawili
Miezi sita iliopita Zinedine Zidane alikuwa akitabasamu alipozungumza kuhusu kufurahia kurudi nyumbani baada ya kurudi kama mkufunzi wa Real Madrid.
Lakini tabasamu hiyo imepotea mara moja kufuatia msururu wa matokeo mabaya msimu huu ambayo yamesababisha presha chungu nzima dhidi ya raia huyo wa Ufaransa.
Baada ya kutoka sare na Real Valladolid katika uwanja wa Bernabeau na Villareal katika ligi ya la Liga , Real ililazwa 3-0 na Paris St Germain katika kombe la vilabu bingwa siku ya Jumatano.
Ni Zidane ambaye alionekana kuwa kocha bora zaidi alipoisaidia Real Madrid kushinda makombe matatu ya klabu bingwa kati ya 2016-2018
Na je ni nani haswa anayepigiwa upatu kuchukua mahala pake?

Je Real Madrid imechoka?

Takwimu za ushindi wa Zidane zipo chini ya asilimia 50 tangu aliporudi katika mji mkuu wa Uhispania karibu na mwisho wa msimu uliopita.
Real imeshinda mechi 7 kati ya 16 za La Liga na zile za ligi ya mabingwa ikitoka sare 4 na kupoteza nne.
''Unatazama kiwango cha joto cha klabu hiyo mtaalam wa kandanda wa Uhispania'', Guillem Balague aliambia BBC radio 5 live.
Wasikilize waandishi walio karibu na rais wa Real na wanapoanza kumfuata Zidane basi ujue mlango upo wazi.
Zinedine Zidane, je muda wake unayoyoma Real Madrid?
Mtaalam wa soka nchini Ufaransa Julien Laurens haamini kwamba Zidane atajiuzulu na kwamba mshindi huyo wa kombe la dunia 1998 anaelewa kile kinachohitajika kuweka mambo sawa.
''Anaamini kwamba kutakuwa na mwangaza mwishowe'', aliongezea Laurens.
''Sio mtu wa kuachilia rahisi anaelewa udhoofu wa kikosi chake . Safu ya kiungo cha kati sio ile ya klabu kubwa. Atalazimka kutiufuta mbinu inayohitajika na jumbe mzuri''.

Je Zidane ataendelea kuifunza klabu hiyo ifikiapo Christmasi?

Real haifanyi mchezo inapofika wakati kwamba mabadiliko yanahitajika.
Walisubiri hadi mwezi Oktoba kumfuta kazi Julen Lopetegui msimu uliopita.
Mkufunzi huyo wa zamani wa timu ya Uhispania aliifunza klabu hiyo kwa miezi mine na nusu.
Aliyechukua mahala pake Lopetegui alikuwa Santiago Solari ambaye alifutwa kazi chini ya miezi mitano akiwa mkufunzi huku mahala pake pakichukuliwa na Zidane aliyerudi katika klabu hiyo mwezi Machi.
Julen Lopetegui alikuwa mkufunzi wa Real Madrid kwa miezi minne na nusu
"Iwapo ana bahati kama ilivyokuwa katika kipindi chake cha mchezo , ataifunza klabu hiyo hadi mwisho wa msimu'' , aliongezea Ballague.
Lakini mienendo ya klabu hiyo ni mibaya na hata kurudi kwa Sergio Ramos, Marcelo na Luka Modric hakutatosha kwa yeye kuwepo hadi Christmas.
Mwandishi wa soka kutoka Ubelgiji Kristof Terreur hana matumaini na Zidane.
Je anaongeza nini katika timu yake? Ana filosofia gani?
Wakati Real Madrid iliposhinda kombe la vilabu bingwa bado haijajulikana waliweza vipi kushinda, alisema Terreur .

Mourinho kuchukua mahala pake Zidane?

Jose Mourinho anahusishwa pakubwa kurudi Bernabeu iwapo Zidane atafutwa.
Mkufunzi huyo wa zamani wa Chelsea ambaye aliondoka Real Madrid 2013 baada ya kipind cha miaka mitatu yupo baada ya anapatikana baada ya kupoteza kazi yake Man United mwezi Disemba 2018.
'Natumai Jose atakuwa akitafuta kazi Novemba', Terreur.
Florentino Perez (kushoto) na Jose Mourinho walikuwa wakitabasamu wakati walipokutanba katika kongamano la Fifa mwezi Juni
"Real Madrid huenda watamuhitaji mtu kama Mourinho ambaye hapendi mzaha.
''Wanahitaji mkufunzi ambaye ataweka nidhamu na kuisaidia timu hiyo.Blague aliongezea: Sote tunajua kwamba Mourinho anasubiri''.

Je ni nini kilichokoseka dhidi ya PSG?

Real ilianza vibaya mechi za ligi ya mabingwa siku ya umatano , huku Angel Di Maria akifunga mara mbili dhidi ya mwajiri wake wa zamani na kuisaidia PSG kupata ushindi muhimu.
Bao la dakika za mwisho la Thomas Meunier liliongeza chumvi katika kidonda.
Je ni nini haswa kilichoharibika kati ya Zidane na wachezaji wake?
''Hakukiandaa kikosi chake vyema kucheza dhidi ya PSG na hayo ni makosa makubwa'', aliongezea Ballague.
Eden Hazard
"Safu ya kati ya Real Madrid ilikuwa imeingia ndani ya uwanja sana huku kukiwa na nafasi kila mahali - hakuweza kusahihisha hilo''.
Kama mkufunzi alifeli kwa mara nyengine. Wanacheza dhidi ya Sevilla siku ya Jumapili na Atletico Madrid mwisho wa mwezi Septemba .
Mechi nne au tano zijazo zitakupatia kipimo cha ni hadi wapi timu yake itafika.
Laurens alisema , Real ilionekana kuchanganyikiwa kuanzia mwanzo hadi mwisho.
''Hawakuweza kucheza hata pasi tatu mfululizo katika safu ya kati, walichezewa kila kitengo''.
Terreur aliongezea: Ninapoitazama Real Madrid ikicheza, inanikumbusha kuhusu Marc Wilmots akiifunza Ubelgiji ambapo kulikuwa hakuna mpangilio wowote.

0 comments:

Post a Comment