Thursday, October 31, 2019



KIKOSI cha Liverpool kimesonga hatua ya Robo Fainali ya Carabao Cup baada ya ushindi wa penalti 5-4.
Mchezo huu ambao umechezwa uwanja wa Anfield ulikuwa na maajabu yake kwani ulikusanya jumla ya mabao 10 ndani ya dakika 90.

Sare ya mabao 5-5 ilipelekea timu hizo kupigiana penalti ambapo Arsenal ilishinda penalti 4 na kukosa moja huku Lierpool ikishinda penalti zote tano.

Wapigaji kwa upande wa Arsenal ni Bellerin, Guenduozi, Martinell hawa walipata, Ceballos alikosa, Maitland- Niles alipata.

Kwa upande wa Liverpool alianza Milner, Lallana,Brewster Origi na Jones alimaliza kwa kufunga penalti ya ushindi.

0 comments:

Post a Comment