Wakati timu ya Lipuli ikitarajiwa kukipiga na Polisi Tanzania leo uongozi wa Lipuli unasikitika kuona Jeshi la Polisi limewakamata wachezaji wetu wanne.
Waliokamatwa ni Paul Nonga, Issa Ngoah, Seif Karihe na Daruwesh Saliboko na kuwapiga, kuwachania nguo na kuwapeleka kituo cha Polisi.
Tukio hilo limetokea leo majira ya saa moja jioni wakati wachezaji wetu kwa pamoja wakitoka katika ofisi za klabu zilizopo nje ya uwanja wa Samora.
Baadhi ya viongozi wa klabu wapo kituo cha Polisi kujaribu kufatilia kwa karibu jambo hili. Uongozi wa Lipuli unalaani vikali vitendo vyovyote ambavyo si vya kiungwana.
Imetolewa na Idara ya Habari na Mahusiano ya klabu ya Lipuli.

0 comments:
Post a Comment