
Bundi yungali juu
ya paa la kocha wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer, hata baada
ya kutoka sare katika mchezo wa jana usiku dhidi ya Arsenal.
Man
United ikiwa nyumbani Old Trafford ilitangulia kupata goli kupitia shuti
kali la kiungo Scott McTominay katika dakika ya 45. Mshambuliaji Pierre-Emerick Aubameyang akawarudisha Arsenal mchezoni katika dakika ya 58, na mpaka dakika 90 zikikamilika matokeo yakasalia 1-1.
- Tetesi za Soka Ulaya Jumanne 01.10.2019
- Solskaer: Mimi ni mtu sahihi wa kuinoa Man United
- Jedwali la Msimamo wa Ligi ya EPL 2019/20
Bada ya kucheza mechi saba, United ipo katika nafasi ya 10, na alama 9 yakiwa ni matokeo mabaya zaidi katika miaka 30, kwa kushindwa walau kufikisha alama 10. Mara ya mwisho United kuwa na matokeo kama haya, 1989-90 walimaliza ligi katika nafasi ya 13.
Kwa mara ya kwanza toka mwaka 2000 Arsenal inanusurika kipigo katika dimba la Old Trafford katika mechi mbili mfululizo za ligi. Pia Arsenal imepiga mashuti mengi zaidi yaliyolenga lango (5) dhidi ya Man United (4) katika dimba hilo toka mwaka 2009.
Arsenal wana alama 12, Man United 9 jumla yao ni alama 21, sawa na alama za Liverpool ambao wapo kileleni.

Solskjaer, amesema, baada ya mchezo huo kuwa wana somo kubwa la kujifunza kutokana na matokeo hayo: "Mara ngapi tumekuwa tukiongoza 1-0 na tumeshindwa kufunga goli la pili? Tuna bonde refu la mambo ya kujifunza, na tutaendelea kufanya kazi kwa bidii, kwa uzoefu zaidi tutafanya maamuzi sahihi."

"Hatukujituma ipasavyo mwanzoni mwa kipindi cha pili. Arsenal walijitoa kwa nguvu na kupata bao," amesema Solskjaer na kuongeza "Nilidhani tungeweza kupachika goli la pili mwishoni mwa mchezo, tulishambulia sana. Nimeshawahi kuwa katika hali kama hiyo nikiwa mchezaji, ambapo
Kwa upande wake kocha wa Arsenal Unai Emery amesema bado anataka matokeo bora zaidi kutoka kwa wachezaji wake: "Tuliingia uwanjani kushindana na tungeweza kufanya vyema zaidi. Tunaweza kumiliki mchezo zaidi na kutengeneza nafasi za kushinda. Tuna wachezaji wadogo ambao wanaweza kujiamini zaidi."
0 comments:
Post a Comment