Shirikisho la soka nchini Uganda (FUFA) limemtanganza kocha mpya Jonathan Mckinnstry ambaye anachukua nafasi ya Sebastian Desabre.
Loading...
Jonathan ambaye ni raia wa Ireland amewahi kuzifundisha timu za taifa za Sierra Leone na Rwanda kwa nyakati tofauti.
Mtihani wa kwanza kwa Jonathan utakuwa ni kuhakikisha Uganda inafuzu kucheza fainali za CHAN 2020 lakini si kufuzu pekee bali kuhakikisha inafanya vizuri kwenye michuano hiyo kwa sababu Uganda kufuzu fainali hizo sio jambo geni kwa sababu tayari imefanya hivyo mara nne.
0 comments:
Post a Comment