Manchester
United imekaribia kukamilisha uhamisho wa mshambuliaji wa Juventus na
Croatia Mario Mandzukic 33 katika dirisha la uhamisho la mwezi Januari.
(Tuttomercatoweb, via Express)

Arsenal, Liverpool na Manchester United wamekuwa wakiwasiliana na jopo la maafisa wa kiungo wa kati wa Uswizi na Borussia Dortmund Denis Zakaria, 22. (Sky Deutschland, via Inside Futbol)
Mshambuliaji wa Manchester City na Brazil Gabriel Jesus, 22, amepinga uvumi unaomuhusisha na Bayern Munich , akiandika katika mtandao wa Instagram kwamba uvumi huo ulikuwa uongo. (Manchester Evening News)

Newcastle iko tayari kumsaini kiungo wa kati mwenye urefu wa futi sita na nchi nne raia wa Ufaransa Ibrahima Sissoko, 21, kwa dau la ya £13m kutoka klabu ya ligi ya daraja la kwanza Strasbourg. (Sun)
Manchester United iko kifua mbele kumsaini Red Bull Salzburg na mshambuliaji wa Norway Erling Braut Halaand, 19. (Corriere dello Sport, via Manchester Evening News)

Everton imekuwa ikimsaka kiungo wa kati wa Czech Republic na Spartak Moscow Alex Kral, 21. (Clubcall)
Mshambulauji wa Ubelgiji Eden Hazard, 28, amefichua kwamba alizungumza na rais wa Real Madrid Florentino Perezmwaka mzima kabla ya kupata uhamisho wa kuelekea Chelsea . (Talksport)
Wachezaji wa Arsenal wanamtaka kiungo wa kati wa Uswizi Granit Xhaka, 27, kusalia kuwa nahodha wa klabu hiyo licha ya kuwatukana mashabiki alipotoka katika mechi iliotoka sare ya 2-2 dhidi ya Crystal Palace siku ya Jumapili.. (Times, subscription required)

Aliyekuwa mshambuliaji wa Manchester United na Sweden Zlatan Ibrahimovic, 38, amesema kwamba huenda akajiunga na klabu ya La Liga kufuatia huduma yake ya miezi kumi na nane akiichezea LA Galaxy. (Metro)
Kiungo wa kati wa zamani wa Tottenham Rafael van der Vaart amekiri kwamba alimwambia mwenyekiti wa Spurs Daniel Levy kumsaini kiungo wa kati wa Ajax na Morocco Hakim Ziyech, 26. (Star)
Haki miliki ya pichaGETTY IMAGES
0 comments:
Post a Comment