Uongozi wa klabu ya Yanga umetangaza majina ya wachezaji ambao wataondoka leo kuelekea Misri kwa ajili ya mechi ya Kombe la Shirikisho Afrika dhidi ya Pyramids FC.
Kikosi kinachoondoka ni makipa, Farouk Shikalo, Metacha Mnata na Ramadhan Kabwili, mabeki ni Juma Abdul, Ally Ally, Ally Mtoni ‘Sonso’, Lamine Moro na Mharami Said Issa ‘Marcelo’
Viungo ni nahodha Papy Tshishimbi, Feisal Salum ‘Fei Toto’ Mapinduzi Balama, Abdulazizi Makame, Deus Kaseke, Jaffar Mohammed huku mawinga ni Mrisho Ngassa, Patrick Sibomana na Issa Bigirimana, wakati washambuliaji ni Sadney Urikhob na Juma Balinya.
Katika mechi ya kwanza ikumbukwe Yanga ilipoteza kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa CCm Kirumba jijini Mwanza.

0 comments:
Post a Comment